Follow Us on Social Media

MAMA ALIYEPOTEA KWA MIAKA 43 AREJEA NYUMBANI NA WATOTO SITANA BONIE

Machozi ya furaha iliwabubunjika wakazi wa Waita eneo la Mwingi ya Kati, baada ya mwanamke, mama wa watoto watatu aliyepotea miaka zaidi ya 40 iliyopita kurejea nyumbani akiandamana na watoto wengine sita.

Agnes Wanza anasemekana kutorokea kusikojulikana kufuatia mizozo ya kinyumbani na mumewe  mnamo mwaka wa 1974 na tangu mwaka huo hakuna aliyejua aliko hadi jana.
AGNES WANZA, MAMA ALIYEPOTEA ZAIDI YA MIAKA 40 ILIYOPITA

Kulingana na Mwikali Katee ambaye ni binti wa kwanza wa Agnes Wanza (mwanamke aliyepoteza) na ambaye hadi sasa amekua bila malezi ya mama hadi akawa Naibu wa Chifu wa kata ndogo ya Mwambui, mama yake aliwaacha wakiwa mchanga sana mwaka wa 1974. Wakati huo, dada yao wa mdogo alikuwa na umri wa miezi 9.

Mwikali alisema migogoro ya kifamilia ndiyo ilisababisha mama yao kutorokea kusikojulikana. Ni hadi Novemba mwaka huu wakati vijana wawili walijitokeza kwenye soko la Waita wakidai kuwa wana wa Agnes Kasyoka, ambaye alikuwa mamake Mwikali.

Hivi ndivyo Mwikali alivyoweza kumtambua mama yake ambaye alikuwa amekwisha kuolewa na watoto wengine sita huko eneo la Kangere, Meru ya Kati.

Moses Kirinya, mwana wa kwanza katika familia nyingine ya Mwanamke huyo huko Meru alisema kuwa wamejaribu kwa muda mrefu sana kuchunguza sehemu ya Ukambani aliyotoka mama yao bila mafanikio, kwani mama yao aliifanya siri kubwa.

"Hatukujua kamwe kwamba mama yetu alikuwa na watoto wengine huku Ukambani, wala  hakutaka kamwe kumwambia mtu yeyote mahali pa kuzaliwa kwake! "Alielezea Kirinya

Mwaka huu walimsihi mama yao angalau awajulishe mahali pake ya kuzaliwa na kwa bahati aliwaambia kuwa alikuja kutoka mahali panapojulikana  kama Waita katika eneo mbunge la Mwingi ya Kati, Kitui ya Kitui. Mnamo tarehe tano Novemba mwaka huu ndipo walianza safari ya kutafuta alikokuwa ametoka mama yao.

Baada ya safari ndefu, waliweza kufika eneo hilo na lililowashangaza ni habari kuwa mama yao alikuwa na watoto wengine watatu na alikuwa ameolewa kwingine kabla ya kukutana na baba yao huko mjini Meru.

"Tulipofika katika soko la Waita, tulishuka kwenye Probox iliyokuwa imetubeba tukawasihi wakaazi watuelekeze kwenye boma la Karanja Munuve, ambaye mama yetu alikuwa amesema  kuwa mjomba wetu. Hapo ndipo tulipata habari kuwa mama yetu alikuwa na watoto wengine watatu na baadaye tukapata nafasi ya kukutana na dada yetu mkubwa Mwikali, "alisema Kirinya.

Mipango ilifanywa ili kuunganisha hizi familia zetu mbili na jana sherehe kubwa ilifanyika katika boma la Mwikali huko kata Ndogo ya Mwambui na wakazi wa eneo hilo wakaja kwa wingi katika boma hilo ili kushuhudia hadithi hii ya mwanamke aliyepotea na kutokea zaidi ya miaka 40 baadaye.

Kwa familia ilikuwa siku bora zaidi maishani mwao kwani walifanikiwa a kuona mama yao kwa mara ya kwanza katika miaka 43 na wengine walipata nafasi ya kuona dada zao na ndugu zao ambao hawakuwa na mawazo kwamba walikuwepo.

Mwisho.

No comments

Post a Comment

© all rights reserved
made with by Skitsoft